Friday, July 28, 2017

VAZI LA SURUALI



Wapendwa!!!  mara kadhaa nimekuwa nikitatizwa sana na vazi la suruali kwa maana hasa ni nani kati ya mwanamume na mwanamke anayestahili, nimekutana na wanazuoni wakiwemo wachungaji ndiyo kwanza wameishia kupingana kwa maana kati yao wamekuwa wakidai suruali ni vazi la kike na miongoni mwao wamedai ni vazi la kiume, kwa hali hii naomba msaada wenu lipi ni jibu stahiki?

Tuesday, September 9, 2014

BARAZA LA MADIWANI LAMTOLEA UVIVU MKUU WA WILAYA - MBOZI

Katika hali isiyoyakawaida baraza la madiwani wilaya ya mbozi ktk kikao chake cha kujadili taarifa (hoja ya mdhibiti na mkaguzi wa serikali, kwa kutumia vibaya fedha ya halimashauri mbapo kwa wastani mkuu huyo wa wilaya amekuwa akitumia tshs millioni 4 kwa wiki mbili hivyo madiwani hao wakieleza kwa uchungu wamedai matumizi hayo ni sawa na karibu millioni 8 kwa mwezi na ikiwa kimsingi ni matumizi binafsi. madai hayo yametilewa na madiwani hao mbele ya mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya Mh. Dr. kadeghe

Thursday, July 11, 2013



KUANZISHA MKOA MPYA MBEYA NI KWA MASLAHI BINAFSI

Hivi karibuni imesikika kupitia kikao cha Ushauri cha mkoa (RCC) kupendekeza kuanzishwa kwa mkoa mpya kwa jina la songwe na kupendekeza makao makuu yake yawe mkwajuni huko chunya. kimsingi ktk zama hizi za mabadiliko makubwa ya kimfumo yayotaka kupeleka zaidi madaraka chini kwa wananchi (grassroot level), haya yanaainishwa vizuri zaidi katika reform ya serikali za mitaa, yenye nia mahususi ya kuona zana ya ushirikishwaji wa wananchi ktk kutumia rslimali walizonazo kuanzia ngazi za chini kabisa inapewa umuhimu mkubwa. kwa hali kama hii nadhani ingekuwa vema zaidi kama badala ya kuanzishwa kwa mkoa mpya basi ingekuwa bora kuanzishwa halmashauri katika wilaya kubwa kama chunya badala ya (Ku - Regionalize), tungali tukijua tatizo ni huduma kwa watu walio pembezoni halmashauri moja imekuwa vigumu kuifikia pande zote. hivyo tatizo la chunya kwa ukubwa wake si kweli kwamba Mh kandoro alikwama kuifikia bali huduma kupitia halmashauri ya chunya hazikuweza kupelekwa kutokana na ukubwa wa kijiografia.

Saturday, May 4, 2013

NINI UNGEKUWA MSIMAMO WAKO??



Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mwesiga Beregu, amekataa kata kata wito wa chama chake wa kumtaka ajotoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,huku yeye akiweka msimamo wake wazi kwamba Tanzania ni muhimu zaidi kwake kuliko chama chake hicho.

Habari zilizoppatikana na kuthibitishwa Profesa Baregu, zinasema katibu Mkuu wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa, alimwiita msomi ambae ni mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akimtaka ajitoe. Ndani ya Tume hiyo kwasababu za kisiasa kwa madai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeuteka mchakato huo.

Profesa Beregu anaelezwa kumjibu Dk Slaa kwa kutumia maneno ya kiingereza, "If I am told to choose between my country and my party (Chadema), I will choose my country", akiwa na maana kwamba kama angetakiwa kuchagua kimoja kati ya nchi yake na chama chake cha Chadema, angechagua nchi yake kwanza.

Akizungumza na Raia Mwema juzi Jumatatu jijini Dar es Salaam, Profesa Baregu amekiri kutoa msimamo huo Katibu Mkuu wake Dk Slaa, pamoja na chama chake cha Chadema, akisema viongozi wenzake hao wanapaswa kujishauri mara mbili mbili kabla ya kuchukua uamuzi huo wa kujitoa ikizingatiwa. Kwamba tangu mwanzo chama hicho ndicho kilichoasisi suala zima la Tanzania kuwa na Katiba Mpya tofauti na hii ya sasa.