Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chama Cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa
Mwesiga Beregu, amekataa kata kata wito wa chama chake wa kumtaka ajotoe
ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,huku yeye akiweka msimamo wake
wazi kwamba Tanzania ni muhimu zaidi kwake kuliko chama chake hicho.
Habari zilizoppatikana na kuthibitishwa Profesa Baregu, zinasema katibu Mkuu wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa, alimwiita msomi ambae ni mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akimtaka ajitoe. Ndani ya Tume hiyo kwasababu za kisiasa kwa madai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeuteka mchakato huo.
Profesa Beregu anaelezwa kumjibu Dk Slaa kwa kutumia maneno ya kiingereza, "If I am told to choose between my country and my party (Chadema), I will choose my country", akiwa na maana kwamba kama angetakiwa kuchagua kimoja kati ya nchi yake na chama chake cha Chadema, angechagua nchi yake kwanza.
Akizungumza na Raia Mwema juzi Jumatatu jijini Dar es Salaam, Profesa Baregu amekiri kutoa msimamo huo Katibu Mkuu wake Dk Slaa, pamoja na chama chake cha Chadema, akisema viongozi wenzake hao wanapaswa kujishauri mara mbili mbili kabla ya kuchukua uamuzi huo wa kujitoa ikizingatiwa. Kwamba tangu mwanzo chama hicho ndicho kilichoasisi suala zima la Tanzania kuwa na Katiba Mpya tofauti na hii ya sasa.

No comments:
Post a Comment