Thursday, July 11, 2013
KUANZISHA MKOA MPYA MBEYA NI KWA MASLAHI BINAFSI
Hivi karibuni imesikika kupitia kikao cha Ushauri cha mkoa (RCC) kupendekeza kuanzishwa kwa mkoa mpya kwa jina la songwe na kupendekeza makao makuu yake yawe mkwajuni huko chunya. kimsingi ktk zama hizi za mabadiliko makubwa ya kimfumo yayotaka kupeleka zaidi madaraka chini kwa wananchi (grassroot level), haya yanaainishwa vizuri zaidi katika reform ya serikali za mitaa, yenye nia mahususi ya kuona zana ya ushirikishwaji wa wananchi ktk kutumia rslimali walizonazo kuanzia ngazi za chini kabisa inapewa umuhimu mkubwa. kwa hali kama hii nadhani ingekuwa vema zaidi kama badala ya kuanzishwa kwa mkoa mpya basi ingekuwa bora kuanzishwa halmashauri katika wilaya kubwa kama chunya badala ya (Ku - Regionalize), tungali tukijua tatizo ni huduma kwa watu walio pembezoni halmashauri moja imekuwa vigumu kuifikia pande zote. hivyo tatizo la chunya kwa ukubwa wake si kweli kwamba Mh kandoro alikwama kuifikia bali huduma kupitia halmashauri ya chunya hazikuweza kupelekwa kutokana na ukubwa wa kijiografia.
Subscribe to:
Posts (Atom)