Katika pitapita zangu siku mbili hizi yaani tarehe 28 na 29, nimeweza kuonana na ndugu na jamaa zangu wengi wao wakiwa katika pilikapilika za hapa na pale, na bahati nzuri nilijaliwa kuwauliza kilichojili na majibu yalikuwa hivi;
Mfanyabiashara wa nyumba ya kulala wageni " Kwa siku hizi mbili namshukuru Mungu kwani nimepata watega wa kutosha" na kwa mfanyabiashara wa mchele alicheka na kudai wateja kwa jana na leo wapo tofauti ktk maana hawasemi nipunguzie zaidi ya kusema nifungie vipeto vya debe tatu kwa watu watatu na kulipa bila kigugumizi" mwisho alieniacha hoi ni wa kitimoto aliyedai mzigo kwa sasa haupatikani na wadau ni wengi, nipotaka kujua wametoka wapi ghafla alijibu kwa mkato haelewi ila wanaonekana ni wageni wengi wao. ndipo nilipokumbuka usemi usemao "Mgeni njoo wenyeji tupone" ugeni mkubwa unaotarajia kuja kesho wa mh Rais na msafara wake kwa namna fulani imegeuka neema kwa waliojipanga vizuri kutumia fursa hiyo ukiachilia mbali kwa baadhi ya wasiutakia mema mkoa wetu kwa maslahi ya msingi kutokana na madai yao lakini yasiyozingatia haki ya upande mwingine na hivyo kuonekana ni binfsi zaidi. Nina hakika wafanyabiashara wakubwa na wadogo Mbeya wamepata wakati mgumu sana wa kuweka mambo yao sawa kwa mahitaji makubwa ya ghafla kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma zao na hivyo kulazimika kuwapoteza wateja kwa mfano wageni kuwapeleka kulala uyole na hotel za mbalizi.
No comments:
Post a Comment