UWEPO WA SERIKALI ZA MITAA
Kwa mujibu wa sheria uwepo wa serikali za mitaa umeainishwa katika ibara ya 145 hadi 146 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 na katika sheria za serikali za mitaa namba 7 ya mwaka 1982 kwa halmashauri za wilaya na sheria namba 8 ya mwaka 1982 kwa halmashauri za miji kwa maana ya manispaa na majiji sambamba na marekebisho yake ya mwaka 2002.
Kwa ufupi halmashauri zinaendeshwa kwa usimamizi wa karibu kupitia mabaraza ya madiwani ambao kimsingi utaratibu wa uendeshaji unaongozwa kanuni za madiwani za mwaka 2000 kwa halmashauri za miji. katika utaratibu huo unaweka wazi kuwa chombo chenye mamlaka ya juu ni baraza la madiwani yaani (full council) sambana na kamati ya fedha na uongozi inayohusisha wenyeviti wa kamati za kudumu kama kamati ya ujenzi na miundombinu, kamati ya Aridhi, mipango miji na mazingira na kamati ya elimu afya na uchumi.
kupitia utaratibu ulioainishwa kisheria unaotaka baraza la madiwani kuwa chombo cha juu chenye mamlaka ya usimamizi wa raslimali na uendeshaji wa halmashauri kumekuwepo na mapungufu makubwa yanayopelekea wajibu wa mabaraza (full council) kutokukidhi, moja ya kikwazo kikubwa ni mamlaka za uteuzi kwa watendaji wake akiwemo mkurugezi (mtendaji mkuu) ambaye kwa mujibu wa sheria anateuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kwa halmashauri za miji na kwa upande wa halmashauri za wilaya huteuliwa na Waziri mkuu jambo ambalo linaleteleza utata katika uhusiano uliopo kiutendaji kwa misingi kwamba katika mazingira ya kawaida wakurugezi wengi wamekuwa wakitii zaidi mamlaka zilizowateua na kujikuta wakitekeleza maagizo tofauti na maazimio ya mabaraza yao, ipo mifano mingi lakini kwa ujumla wake hupelekea matumizi mabaya ya raslimali na hatimae migogoro isiyokwisha haswa ukizingatia kuwa wakurugenzi wengi wanajikuta wanawajibika kuwatumikia mabwana wawili na hatime kushindwa kuwa na misimamo makini. Pili lipo tatizo la uwajibikaji kwa dhana ya uwasilianaji (reporting system) kwa wakurugenzi wetu katika mazingira ya mwingiliano wa kisecta kwani upo wakati mkurugenzi anawajibika kutoa taarifa kwa vyombo vingine kama wizara ktk maana ya serikali kuu kwa utaratibu utakaokuwa umeainishwa na wizara husika kwa utarabu wa serikali kuu bila kuzingatia matakwa na uhitaji wa sheria inayosimamia serikali za mitaa kwa maana ya sheria ya fedha, na sheria mbali mbali ndogo zilitungwa kwa kuzingatia mazingira ya halmashauri husika.
Mapendekezo katika matatizo yanayojitokeza kwa halmashauri zetu ni kama ifuatavyo;
Mamlaka za uteuzi kwa halmashauri zetu zirudishwe kwa mabaraza husika kwa utaratibu wa ajira kwa ngazi za wakurugenzi serikali kuu itoe miongozo ya sifa na swala la uajiri liachwe kwa baraza la madiwani ambao ndiyo chomba simamizi kwa halmashuri. na kwa upana huu ni vema pia serikali ione uwezekano wa wenyeviti wa mabaraza haya kuchaguliwa na wananchi wote wa halmashauri husika badala ya sasa kuachiwa madiwani kufanya jukumu la kumpata mwenyekiti husika. kwa kufanya hivyo nina amini kuwa tutkuwa tumempunguzia Mh Rais mzingo mkubwa wa lawama anazozipata hivi sasa kutokana na uozo mkubwa miongoni mwa halmashauri zetu ikiwemo kutokuwachukulia hatua za kisheria kwa wakati wanapokuwa wameenenda tofauti na maadili ya kiutumishi. kumbuka kwa mfumo tulionao sasa hata kama chama chochote kikapata nafasi ya kuongoza nchi hii tatizo la usimamizi kwa halmashauri zetu likiwemo hili la uteuzi likibaki kuwa mikononi mwa chombo kingine nje ya chombo kinachosimamia kwa karibu halmashauri zetu.
Nitaendelea wiki ijayo
No comments:
Post a Comment