Twiga ni mnyama mpole na mtulivu na ndiyo maana amechukuliwa kama alama maalum ya nchi yetu katika maana nchi yenye amani na uvumilivu
uvumilivu ni sifa pekee ya watanzania ingawa siku za hivi karibuni tunaona uvumilivu unapotea na dalili hizi tunaziona kama vile watu kushindana kihoja haipo tena, imebaki kutishiana kwa misingi ya kwenda kuandamana, tumeshuhudia vingozi wetu wawakilishi kutukana matusi bungeni, tumeshuhudia kiongozi kutetea maovu, maandamano kati ya kundi moja zidi ya lingine. kimsingi viongozi wetu wamekosa uvumilivu, wamenyimwa uzalendo, maslahi binafsi kama kuchoma lami nk
No comments:
Post a Comment